Wednesday, 16 March 2016

Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga


Huyu dada nimemfahamu miaka mitatu iliyopita.

Ni mwanasheria kwenye firm fulani jijini Dar, nilikuwa nina mpango wa kumuoa haraka, ila mmoja wa marafiki zake wa karibu aliniambia nijitahidi kumfahamu kwanza kabla sijaamua kumuoa nadhani alihisi kitu.

Kufahamiana naye kwa muda tukaishia kupata mtoto mmoja wa kike ambaye sasa ana miaka miwili.

Ni mwanamke mzuri sana, ni gumzo kila anapopita au kufanya kazi, hata nilitaka nitoane macho na patina mmoja wa firm yake. 

Kwa kweli anaita kila jicho ana mengi mazuri, lakini pia ana mapungufu yaliyonipigisha breki kali juu ya tope.

Kwa sasa anaishi na wazazi wake, lakini mara nyingi saba tunalala kwangu. Nafahamika kwao kama mzazi mwenza, kwetu pia kaskazini wanamtambua.

Amekuwa ni mwepesi sana wa kupata marafiki wa kiume, ana hasira za karibu, kujiachiachia sana kwa wanaume imekuwa sehemu ya maisha yake, yeye anadai si wapenzi wake. Wanataniana tu hii ni moja ya sababu iliyonizuia kumuoa.

Nilihisi kama hajiheshimu.hayuko tayari kuishi kama mke wa mtu nikadhani nimwache kwanza ale maisha wakati nami nakula taratibu ingawa nahofu ya magonjwa.

Simu zake sijawahi ziona hata mara moja zikiita kwa sauti toka nimfahamu.anashinda watsapp 24/7. 

Facebook kwake ni kama oxgen, kila siku anaongeza wanaume, viber anatumiwa mioyo na mikisi ya wanaume, linkedin pia hayuko mbali.

Nahisi kweli atakuwa ananipenda, lakini kwa hayo nashindwa kuji commit, ila bahati mbaya nashindwa hata kumuacha, hasa ukizingatia nina mtoto naye. 

Yaani sijui nifanyeje, nimbwage.

Naona sio waifu matirio.

Ataniua jamani.

Anashinda Whatsapp Masaa Yote, Ila Nashindwa Kumbwaga Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin