Wednesday, 6 January 2016

UCHAMBUZI YAKINIFU WA RAY NA POZI ZAKE HIZI WAZUA MJADALA HUMU SOMA UTOE MAONI YAKO>>
Miaka takribani 15 iliyopita nyota za Muigizaji Ray na marehemu kanumba zilitawala medani ya tamthilia hapa bongo wote wakiwa ni zao la tanuru lililopika vipaji vingi katika sekta ya uigizaji la kundi lililojihusisha na tamthilia lililoitwa Kaole group.
Mbali na mafanikio ya kuweza wote kumiliki makampuni ya kutengeneza filamu na kuibuka kwa ushindani mkubwa baina yao wawili lakini haina shaka kwa mpenda burudani ya filamu hapa nchini hakika mzani wa kuwapima ray na kanumba usingeweza kukaa katika msawazo kwa maana ya mafanikio makuu ya Marehemu kanumba ya kuanza kujitahidi kuifikisha tathinia ya filamu kimataifa kwa kuweza hata kufanya muvi mbili tatu na wasanii wengine gwiji wa Afrika magharibi toka soko la filamu la nigeria liitwalo nollywood.


Rest In Peace Kanumba:: Hatimaye baada ya wanaburudani kupata pigo zito la kifo cha nguli wao aliyeanza kuonyesha dalili za kuwatoa kimasomaso katika medani za kimataifa kufifia baada ya mwenyezi mungu kumpenda zaidi!! Fikra za watu na jicho la matumaini yakabaki kwa mshindani waliyekuwa wakijaribu labda kukivaa kiatu kimoja na si mwingine ni Ray lakini alahaula ni miaka inayoyoma na katika peruzi peruzi zangu na kumbana na picha za mkali wa bongo muvi akiwa katika pozi hizi....... Je lile jina la "The greatest" ambalo lilizua mjadala baina yao ndio kusema mwenye nalo kashapumzika kwa amani na Ray kashindwa kulienzi kwa kuwakilisha njia za swahiba wake katika kuivusha sanaa ya bongo kwenye filamu katika soko la kimataifa? hahahaha mpendwa msomaji changia wazo lako kwa ku comment mi nalamba lipsi hapa kidogo.

UCHAMBUZI YAKINIFU WA RAY NA POZI ZAKE HIZI WAZUA MJADALA HUMU SOMA UTOE MAONI YAKO>> Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin