Thursday, 28 January 2016

Range la Wema layeyuka


WEMA37 (1)   Staa wa muvi za Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (kushoto) akiwa na gari yake gari aina ya Range Rover Evogue siku ya kuzaliwa
DAR ES SALAAM: Staa wa muvi za Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye hivi karibuni akisherehekea bathidei yake (siku ya kuzaliwa) alijitapa kujinunulia gari aina ya Range Rover Evogue kwa shilingi milioni 200, sasa inadaiwa kuwa, gari hilo halimiliki tena.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kilichopo karibu na staa huyo, licha ya mwanadada huyo kujitapa kila kukicha kwa kumiliki mkoko huo ambao mara kadhaa kumekuwa na madai ya kwamba alihongwa, kwa sasa hayupo nalo tena na eti imebaki stori tu.
WEMA38.JPG
Muonekano wa nyuma wa Range Rover Evogue hiyo.
“Niwapashe wadaku, lile gari la bi shosti Wema alilojigamba kulinunua kwa jasho lake kwa shilingi milioni mia mbili, sasa hivi wala hayupo nalo. Alilipeleka gereji kufanyiwa matengenezo kisha akalipeleka yadi maeneo ya Kijitonyama kwa ajili ya kulipiga bei.

“Nimeisahau ile yadi lakini lile gari nyinyi si mnaijua, kama mkifanya utafiti wenu kwenye sehemu mbalimbali wanazouza magari za maeneo hayo lazima mtalikuta tu,” aliongeza sosi huyo.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, mapaparazi wetu walichanja mbuga na kuzunguka kwenye gereji mbalimbali zilizopo Kijitonyama lakini halikuonekana. Pia, mapaparazi wetu walikwenda kwenye yadi ya kuuza magari iliyopo Kijitonyama, Dar lakini halikupatikana.
Ili kujiridhisha zaidi, wiki iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwa Wema, Mbezi ya Ununio jijini Dar na kuangalia ndani ya nyumba hiyo ambapo gari hilo halikuwepo. Hata mfanyakazi aliyekutwa ndani ya mjengo huo alipoulizwa, alisema hana jibu lolote kuhusu gari hilo ila akitafutwa Wema itakuwa vizuri zaidi.
Juhudi za kumpata mlimbwende huyo ziligonga mwamba kwa kuwa, mapaparazi wetu walipofika nyumbani kwake hawakumkuta na hata walipojaribu kumtafuta kwa njia ya simu iliita bila kupokelewa hadi gazeti hili linakwenda mtamboni.
Wakati huohuo, vile vijembe kati ya Wema na mzazi mwenzake Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ vinaendelea baada ya majuzi, Zari kupachika maneno kwenye kituo kimoja cha redio akisema; Wema ungekuwa mzuri tungehama mjini.’
WEMA39.JPG
Muonekano wa ndani.
Lakini akiwa anasema hivyo, baba mtoto wake, Diamond au baba Tiffah alibandika kwenye mtandao wake wa Instagram maneno haya; ustaa mjini ni kuwa na nyumba.’
Team Wema walisema maneno hayo yote ni uchokozi kwa Wema ambaye kwa sasa ametulia akilea mimba yake.
Diamond alipoulizwa juzi na gazeti hili kuhusu kuendeleza vijembe kwa Wema alicheka sanaaa! Hata hivyo, vijembe hivyo havioneshi kumtikisa Idris Sultan ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya mababa wawili (na kigogo mmoja) wa mtoto wa Wema aliye tumboni.
WEMA40.JPG
Wema akiwa ndani ya gari lake.
Kwa sasa, Idris anazidi kuchanja mbuga ‘akimhendo’ Wema kimahaba akiamini mimba hiyo ni yake licha ya vyombo vya habari kuanika kuwa, kigogo huyo naye anasema ni yake.
Idris alitupia kwenye mtandao wake wa Instagram picha zake akiwa na Wema katika mapozi ya mahaba huku akisema anampenda sana.
Alipotafutwa na gazeti hili juzi, simu yake iliita kwa muda mrefu lakini haikupokelewa

Range la Wema layeyuka Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin