Friday, 15 January 2016

HAWA HAPA NDIO WATOTO WA MASTAA WA BONGO WANAOSUMBUA KWENYE MITANDAO YA KIJAMIITiffah wa D

Tiffah wa Dimond.
NA MWANDISHI WETU
WATOTO wamekuwa wakileta furaha kwa walio wengi, wawe walio kwenye ndoa au hata wale ambao wako kwenye uhusiano wa kawaida.
Hali hiyo imesababisha kila anayebahatika kuitwa mama au baba kutumia nguvu kubwa kuufahamisha ulimwengu kuwa na yeye ana uwezo wa kuzaa.
mtoto wa kiba

Mtoto wa Kiba.

Katika hili wapo mastaa ambao wanapojaaliwa kuwa na watoto, hutumia muda wao mwingi kuwatangaza kwenye mitandao ya kijamii kila wakati. Mastaa wengi, kama ni mwanamke akijifungua lazima ataanza vurugu mtandaoni, ataposti kampakata, mara anamlisha. Yaani ilimradi kuonesha tu furaha aliyonayo.
Maleeka-FAMaleeka wa Mwana FA.
Kama ni mwanaume, mpenzi wake au mkewe akijifungua, kila wakati atapiga picha za mapozi na kuzitupia mtandaoni. Hii yote ni kuwarusha roho wenzao sambamba na kuonesha ni jinsi gani watoto hao wamewaongezea furaha katika uhusiano wao.
PAULA-P-FUNK

Paula wa Kajala.
Wiki hii katika makala haya nimekuandalia watoto 10 wa mastaa wa Bongo ambao picha zao hazikauki mtandaoni. Katika hao, wapo waliofunguliwa na wazazi wao kurasa kwenye Instagram na Facebook kama vile mtoto wa Diamond, Tiffah, Tanzanite na Patrick.
IMG_5878

Tanzanite wa Hbaba.
Mbali na hilo, wapo ambao wanawaandaa watoto wao kuwa mastaa wa kesho kwa kuwasukumizia kwenye fani f’lani mapema kabisa. Kwa mfano, mtoto wa H. Baba anaonekana kupendelea uigizaji na muziki.
Patrick-Muna

Patrick wa Muna.
Patrick wa Muna naye ni muigizaji mzuri tu.
Genius Boss Ngasa
Tiffah, baba yake aliwahi kusema anapenda aje kuwa mwanamuziki. Yule wa Chuchu Hans ni muigizaji mzuri na Paula wa Kajala anaelekea kwenye uanamitindo.

<<next 1>>

<<HAPA>>

<<Next 2>>

HAWA HAPA NDIO WATOTO WA MASTAA WA BONGO WANAOSUMBUA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin