Tuesday, 12 January 2016

Daktari Amtwanga Ngumi Mgonjwa na Kumuua


daktariDaktari akimpiga ngumi mgonjwa huyo.
Moscow, Urusi
Kanda ya video ya CCTV imesambaa mitandaoni ikimuonesha daktari mmoja aliyefahamika kwa jina la Ilya Zelendinov nchini Urusi alimpiga ngumi mgonjwa Yevgeny Bakhtin (56) na kumuua papo hapo.daktari (5)
Kisa hicho kilitokea katika Mji wa Belgorod umbali wa kilomita 670 Kusini mwa Mji Mkuu wa Moscow nchini Urusi mnamo Disemba 29.
daktari (4)Kisa kilianza kwa mgonjwa huyo kumpiga teke muuguzi mmoja kabla ya daktari huyo kumfata na kumpiga ngumi ya kichwa.
daktari (3)Hali ya taharuki
Vyombo vya habari vya Urusi vimeeleza kuwa, baada tu ya kupigwa ngumi mgonjwa huyo alizirai kabla ya kuaga dunia muda mfupi baadaye akiwa hospitalini hapo.
daktari (2)
Wachunguzi wanadhani kwamba hakumuua kwa makusudi lakini wameanzisha kesi ya uhalifu dhidi ya daktari huyo na endapo akipatikana na hatia atapelekwa jela kosa la jinai.
daktari (1)Mgonjwa baada ya kuzirai.
Angalia video ya tukio hilo.

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

Daktari Amtwanga Ngumi Mgonjwa na Kumuua Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin