Monday, 4 January 2016

Aika na Nahreel wa Navy Kenzo Wafunguka..Tuliamua Kuanza A Bila Kuwategemea Wazazi..Tulilala Chini Kwenye Kagodoro

Members wa Kundi la Navy Kenzo linalofanya Vizuri katika mziki ndani na nje ya Tanzania wamefunguka kwa ufupi jinsi walivyoanza maisha yao ya muziki mpaka kufikia hapo walipo

Waimbaji hao ambao ni wapenzi wamesema walikutana India masomoni walipokuwa wakisomeshwa na Wazazi wao na baada ya kumaliza Waliamua Kufanya kazi huko lakini Baada ya Kuona vipaji vyao vinapotea bure wakaamua kuja Tanzania ili kuendelea na muziki na ndio hapo kundi la Paone lilipoanzishwa wakiwa vijana Wanne

Lakini baada ya muda kundi la Paone lilisambaratika na hapo ndipo ukawa mwanzo mzuri wa kundi lenye mafanikio la Navy kenzo liliundwa na Aika na Nahreel,

Maisha yao walipofika Dar es Salaam kwa Mara ya Kwanza wakitokea India Masomoni yalikuwa chini sana kiasi cha kulala chini kwenye Kagodoro kadogo huku Nahreel akifanya kazi ya kutengeneza Beat na Aika Akijishughulisha na Mambo ya Urembo, Aika Anasema waliamua ku take risk na kuanza upya from the scratch ili waweze kuwa na kitu cha kujivunia baadae walichokifanya wenyewe bila kuwategemea wazazi wao ambao kwa kupindi hicho walikuwa na uwezo wa kuwasaidia kwa chochote lakini waliamua kufanya yao na sasa kufika hapa walipo kama moja ya kundi bora la muziki kuwahi kutokea Tanzania.

Kwa sasa wawili hawa wanamiliki kampuni na Studio ya mziki inayojulikana kama "The Industry"

<<NEXT 6>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 2>>

<NEXT 1>>

Aika na Nahreel wa Navy Kenzo Wafunguka..Tuliamua Kuanza A Bila Kuwategemea Wazazi..Tulilala Chini Kwenye Kagodoro Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin