Monday, 28 December 2015

PEDESHE AAPA KUVUNJA UCHUMBA WA DIDAPedeshee maarufu jijini Dar anadaiwa kuapa kuvunja uchumba wa Mtangazaji wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ mara tu baada ya kutangaza kuvalishwa pete ya uchumba hivi karibuni na mwanaume ambaye hakutaka kumuanika.
 IMG_20151212_185836
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini zilieleza kwamba, pedeshee huyo amekuwa akimpa Dida vitisho kuwa mwanaume ambaye atamuoa hatakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake hivyo anaamini yeye ndiye anayeweza kumpa chochote anachotaka na si mwingine.

“Jamaa anajitapa hata kwa baadhi ya ndugu wa Dida kuwa mwanaume ambaye anataka kumuoa Dida hana vigezo vya kuweza kutatua matatizo yake hivyo yeye yupo tayari kuvunja uchumba huo kwa gharama yoyote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta mtangazaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikiri kujitokeza kwa mwanaume huyo lakini alisema kuwa mwanaume anayemuoa anaweza kukidhi mahitaji yake.
“Mchumba wangu ni mtu mwenye maisha yake wala si mbabaishaji kama baadhi ya watu wanavyodhani na wala sihitaji kabisa ofa ya mwanaume mwingine yeyote,” alisema Dida.

PEDESHE AAPA KUVUNJA UCHUMBA WA DIDA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

1 comments:

LinkWithin