Friday, 13 November 2015

ZUNGU AMKIMBIA SAMWEL SITTA,NI SUALA LA USPIKA,AJITOSA UNAIBU SPIKA,UTITIRI WA MAKADA WA CCM KUJITOSA USPIKA WASHIKA KASI,


ALIYEKUWA mwenyekiti wa Bunge la kumi,Mussa Hassan Zungu ameikataa nafasi ya uspika badala yake ametangaza rasmi kujitosa nafasi ya naibu Spika wa bunge la kumi na moja.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
    Hayo yamebainika Leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mbunge huyo mteule wa Jimbo la Ilala alipokuwa anachukua fomu ya kuwania za nafasi ya uongozi wa Bunge kupitia ndani  ya chama cha Mapinduzi CCM,katika ofisi ndogo za chama hicho zilizoko Lumumba jijini hapa.
     Ambapo Zungu amewaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kutafakari kwa kina ameona nafasi anayoiweza ya kuongoza kwenye Bunge hilo ni nafasi ya unaibu spika tu.
      “Nimekushachukua fomu na sasa nimezirudisha,na nafasi pekee niliyoamba ni Naibu spika na sio uspika,natumaini nafasi hiyo nitaiweza ili niweze kulisimamia Bunge vizuri”amesema Zungu.
     Mbali na Zungu,makada wengine waliojitokeza kuchukua fomu hizo ili waweze kupata ridhaa ya kuliongoza Bunge hilo linatarajiwa kuanza jumanne ya wiki ijayo ni Mbunge mteule wa jimbo la Kasuru mjini,Danel Nsanzugwako.

       Kubuka huku kwa makada hawa wawili mpaka mda huu kunazidi ongeza idadi ya wanaowania uspika kupitia CCM,ambapo mpaka sasa wamefikia 23  wanaojitokeza kuwania  nafasi ya Uspika na naibu spika

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

ZUNGU AMKIMBIA SAMWEL SITTA,NI SUALA LA USPIKA,AJITOSA UNAIBU SPIKA,UTITIRI WA MAKADA WA CCM KUJITOSA USPIKA WASHIKA KASI, Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin