Friday, 6 November 2015

RAIS MAGUFULI, WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WANAKUSUBIRI UWASAIDIE KWA HILI


Nachukua nafasi hii kwanza kumpongeza Rais mpya wa Tanzania Mh. John P. J.Magufuli aliyeapishwa hivi leo. Namtakia kazi njema na kila la heri katika kutimiza majukumu na ahadi zake.

Pili,nawasilisha jambo la muda huu tulionao linalohitaji ufumbuzi wa haraka wa kiserikali. Imesharipotiwa kuwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wamekosa mikopo. Wanaelekea kukwama kupata elimu yao ya juu kwakuwa wengi wao wanatokea familia za kipato cha chini.

Mh. Rais Magufuli,wanafunzi wa vyuo vikuu wana imani kubwa nawe na Serikali utakayoiunda. Wanakusubiri uwasaidie kutatua matatizo yao ya mikopo kama ulivyoahidi ulipokuwa ukipiga kampeni zako. Hakika,wanafunzi wa vyuo vikuu,hasa wale wa mwaka wa kwanza,wanahitaji suluhisho la mikopo yao ya elimu ya juu haraka iwezekanavyo.

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

RAIS MAGUFULI, WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WANAKUSUBIRI UWASAIDIE KWA HILI Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin