Friday, 13 November 2015

BAADA YA WAZIRI HUYU KUKOSA UBUNGE CCM, SASA AUNGANA NA MBUNGE WA CHADEMA..HII HAPA TAARIFA RASMI

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema pamoja na kuanguka kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, bado anayo nafasi ya kushiriki kuleta maendeleo ya Jimbo la Mbozi.

Zambi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, alisema hatosita kutoa ushirikiano pale atakapohitajika na mbunge mpya wa jimbo hilo, Pascal Haonga aliyeshinda kupitia Chadema.

Zambi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbozi kwa vipindi viwili na kuingia katika kinyang’anyiro kuwania muhula wa tatu, alisema anayo nafasi kubwa ndani ya jamii na hivyo anayo fursa ya kuendelea kushirikiana na wananchi.

“Sitosita kumpa ushirikiano mbunge wa Chadema. Lengo letu ni moja kuwaletea maendeleo wananchia,” alisema.

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

BAADA YA WAZIRI HUYU KUKOSA UBUNGE CCM, SASA AUNGANA NA MBUNGE WA CHADEMA..HII HAPA TAARIFA RASMI Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin