Monday, 19 October 2015

WAPINZANI WAJIANDAE KISAIKOLOJIA KUSHIDWA...TAKWIMU HAZIDANGANYI HATA KIDOGO

Kwa namna ya hali ya kampeni inavyoendelea, ni wazi kuwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dr John Pombe Magufuli ni Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayesubiri kuapishwa..

TAKWIMU zifuatazo zinaweka bayana ukweli huo;

- Mgombea wa CCM ndugu John Pombe Magufuli ameshatembea Kilometa 44, 467 katika majimbo 241 ndani ya mikoa 30, ambapo ametumia gari na boti wakati Mgombea wa Ukawa ametembea Kilometa zisizodizi 3,000 kwa gari, ametembelea majimbo 137 yaliyo kwenye mikoa 25.

- Jumla ya mikutano rasmi ya hadhara ni 252 na mikutano midogo ya kusalimia njiani zaidi ya 896 ndio ambayo ameshahutubia Dr John Pombe Magufuli, ukilinganisha na Mgombea wa UKAWA ambae amehutubia Mikutano Mikubwa 102 tu tangu kuanza kwa kampeni na idadi ya mikutano isiyo rasmi ambayo haipo kwenye ratiba ya kusalimia wananchi ni michache sana kwa sababu mgombea huyu anatumia Chopa, hivyo kukosa fursa ya kusalimia wananchi vijijini.

- Ndugu John Pombe Magufuli ameshahutubia kwa masaa takriban 306 sawa na wastani wa 45min - 1hour kwa kila mkutano mkubwa wa hadhara wakati mgombea wa UKAWA amehutubia kwa masaa 26 sawa na dakika 8.93 - 12 kwa kila mkutano.

- Dr Magufuli amekadiriwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 12 ana kwa ana na takriban Milioni 36 kwa njia za Mawasiliano ya Radio, Magazeti, TV na mitandao ya kijamii..wakati mgombea wa UKAWA amewafikia wananchi wasiozidi milioni 5 ana kwa ana katika Mikutano ya hadhara michache aliyoifanya na amewafikia wananchi wasiozidi milioni 11 ktk njia za TV, Magazeti, Radio na mitandao ya kijamii ambapo mara zote mikutano ya UKAWA hairushwi live kwenye TV, wala radio.

- CCM ina wanachama zaidi ya milioni 8 nchi nzima, UKAWA wana wanachama milioni 4 nchi mzima…ikiwa wanachama wa CCM wanaoamini ktk LOWASSA watampigia kura, CCM inakadiriwa kupoteza kura laki nane (ingawa historia inatufundisha kuwa wanaccm huwa wagumu sana kumchagua Kada mwenzao pindi akihama Chama, kumbuka Mrema – 1995)…na ikiwa wanachama wanaoamini katika Lipumba, Makaidi, Mtikila, Dr Slaa na Zitto wataamua kuchagua Uadilifu wa Magufuli, CCM inakadiriwa kupata kura zaidi ya Milioni moja na nusu kutoka kwa wanachama wa Upinzani.

- CHAMA…mtandao wa CCM unaofika ngazi ya nyumba kumi za kila mtaa wa Tanzania na mfumo imara wenye mahusiano mazuri na “system” unamuhakikishia Magufuli ushindi ambapo Mfumo dhaifu uliotokana na Ombwe la uongozi ktk Upinzani unaoamini matusi, vurugu, kashfa na kuimarisha Uadui dhidi ya “system” unaharibu na kufuta kabisa hata yale matumaini kidogo ya kupata hata theluthi ya kura kwa Edward Ngoyai Lowassa.

- Voters Behavior, kwa kawaida CCM inapigiwa kura na wanawake zaidi kuliko jinsia nyingine na makundi rika mengine. Wanawake waliojiandikisha ni Milioni 11,950,200 sawa na asilimia 53 ya watu wote waliojiandikisha, idadi hiyo ni milioni mbili zaidi ya wanaume ambao ni Milioni kumi tu, ambapo kwa kundi rika walio chini ya miaka 30 (yaani Vijana) ni milioni 4 tu.

Mnakaribishwa kwa mjadala hasa kwa wale wenye facts

By Juliana Shonza/JF

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

WAPINZANI WAJIANDAE KISAIKOLOJIA KUSHIDWA...TAKWIMU HAZIDANGANYI HATA KIDOGO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin