Sunday, 25 October 2015

Vijana wa Kiume wanaojihusisha na ushoga wakimbilia Hospitalini kupata matibabuUSHOGA ni haramu kwa jamii nyingi za Afrika zinazozingatia mila na desturi zake. Pia ni dhambi kwa jamii zinazoishi kwa misingi ya imani za dini mbalimbali. 
Tanzania kama nchi haina dini, lakini Watanzania wana dini, hivyo ni dhahiri hawakubaliani na watu wa jinsi moja kuingiliana kimaumbile au watu kufanya vitendo vya kuingiliana kinyume na maumbile.
Lakini ni kweli kwamba wapo watu ambao wanashiriki matendo hayo, pamoja na jamii kuwaona kuwa wamekengeuka.
Kwa nyakati tofauti, watu wa kada tofauti wakiwamo viongozi wa kitaifa wamesikika wakielezea wasivyokubaliana na kuruhusiwa uwapo wa ndoa za jinsi moja nchini.
Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini ambazo zimethibitishwa na madaktari, zinasema kwamba vijana wa kiume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja wameanza kujitokeza katika vituo vya afya kupata tiba kutokana na madhara mbalimbali waliyoyapata.
Baadhi ya waganga hao ameithibitishia FikraPevu kuwekuwepo na wimbi hilo kubwa la vijana wa kiume kukimbilia kwenye vituo hivyo kupata huduma za afya ikiwemo ushauri nasaha, ambao unatokana na matukio ya kunyanyaswa na jamii.
Kwa mujibu wa Dkt. Chikomo John ambaye ni Mratibu wa Afya ya Msingi katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, amesema kundi la vijana hao wanapofika hospitalini wanapopimwa hugundulika kuwa na magonjwa ya ngono (MSM).
Dk. John, amesema wanaojihusisha na ngono ya jinsia moja ndio wanaopata maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia kubwa mara kwa mara licha ya kuwa wanapata matibabu ya maradhi hayo kama walivyo wagonjwa wengine.
Kundi la vijana wanaobalehe linalojumuisha wavulana wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19 ndilo linaloanza kuchipukia kujihusisha na ushoga.
Amesema eneo la haja kubwa limeumbwa kutoa na si kuingiza. Hivyo kitendo hicho husababisha uharibifu na kulegea kwa misuli kwa wanawake na wanaume.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na wimbi la wanaume ambao wamekuwa wakifanya mapenzi kinyume na maumbile na pindi wanapo pata madhara hukimbilia katika vituo vya afya kikiwemo cha Magomeni, Kinondoni Hospitali na Mwananyamala Hospitali ambapo amesema tatizo hilo limewaathiri vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
Baadhi ya vijana wanaojihusisha na ushoga wamesema sababu inayowafanya wafanye mapenzi kinyume na maumbile tofauti na tamaduni za kiafrika ni kujikimu kimaisha. 
Mmoja wa vijana hao ambaye hakuwa tarayi jina lake litajwe mtandaoni (27) mkazi wa Sinza, amesema kazi hiyo inampatia kipato cha kuendesha maisha yake ya kila siku na kuishi sehemu aitakayo licha ya kwamba amewahi kuugua ugonjwa wa Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UIT).
Ameeleza kuwa ufanyaji wa mapenzi kwa njia hiyo upo wa aina nyingi na kuwa wengine hufanyia mdomoni, inategemea na makubaliano. Amebainisha kuwa yeye kama mwanaume ambaye hufanya mapenzi kinyume na maumbile anajua kwamba anaathirika kwa kuacha kufurahia tendo hilo kwa njia ya kawaida na mwanamke lakini kwa mwanaume anafurahia.
Akielezea jinsi anavyoweza kushiriki tendo hilo, amesema anaweza kufanya kwa mkumbo (na mwanaume zaidi ya mmoja). Maradhi mengine ambayo hujitokeza katika sehemu ya haja kubwa pindi mtu anapofanya mapenzi kwa njia hiyo hayana tiba.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam akiwemo Amiri Salim (48) akizungumzia tatizo hilo amebainisha kwamba kukua kwa sayansi na teknolojia duniani na Tanznaia ikiwa tegemezi, ni hatari sana hususani linapokuja shinikizo kutoka nchi za Magharibi, hivyo serikali haina budi kujipanga na kutoa elimu zaidi kupitia taasisi za kidini ili umma uzidi kuona vitendo hivyo ni chukizo mbele za Mungu.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alikaririwa na FikraPevu akisema jopo la watafiti kutoka NIMR katika ripoti yao iliyotoka mwaka 2013 waligundua kuwa chanzo kikubwa kinacho wapelekea wanawake kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na wengine kuogopa kupata mimba.
Aidha, baadhi yao akiwemo aliyejitambulisha kwa jina moja la David, alipohojiwa kuhusiana suala hilo alisema anafanya kwa ajili ya kupata raha tu licha ya kwamba ni jambo linalokatazwa na dini zote na kuwa baadhi yao wamepata maaambukizi ya VVU na sasa wanaenda kupatiwa matibabu katika vituo maalumu.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Azizi Msuya, amesema pamoja na mambo mengine kitendo hicho licha ya ukweli kuwa hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubw kwa mwanadamu, ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.
Amesema wanaopata maambukizi ya virusi vya ukimwi hupewa dawa mbalimbali ikiwemo, Anti Retroital Drugs (ARV’s), Fluconozote tabs, Metronidazole tabs na Clotrimazole pessanes for cream tabs.
Katika Makala zijazo, tutazungumzia tatizo hili jinsi linavyotazamwa na jamii mbalimbali nchini na jinsi waathirika wanavyohitaji kuchukuliwa na jamii, maisha yao, nafasi ya viongozi wa dini, Mazingira yanayowafanya kuchagua kituo/hospitali za kupata matibabu na mengineyo.

Vijana wa Kiume wanaojihusisha na ushoga wakimbilia Hospitalini kupata matibabu Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin