Tuesday, 27 October 2015

Silaha za Kijadi Zakamatwa Shinyanga..Inasemekana ziliandaliwa Kwa Ajili ya Kufanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidiziJustus Kamugisha akionesha moja ya mapanga yaliyokamatwa na jeshi la polisi yanadaiwa kuwa yaliandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu 2015

Vipande vya nondo na mapanga yanayodaiwa kuwa ni ya mgombea ubunge jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Jeremia Mshandete wa Chadema, ni miongoni mwa silaha za jadi zilizokatwa ambazo zinadaiwa kuwa ziliandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu wakati na baada ya uchaguzi mkuu 2015.
Mawe, viroba na makombeo yaliyokamatwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa ndani ya begi na vingine kwenye maboksi kwa ajili ya uharifu katika uchaguzi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi Justus Kamugisha akionesha bendera ya CCM iliyochanwa mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akionesha makombeo yanayoadaiwa kuwa yalilenga kutumika kufanyia vurugu kwenye jimbo la Solwa

Silaha za Kijadi Zakamatwa Shinyanga..Inasemekana ziliandaliwa Kwa Ajili ya Kufanya Vurugu Wakati wa Uchaguzi Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin