Thursday, 1 October 2015

IYOBO AKUBALI KUMUACHIA MTOTO MUME WA AUNT

Shani Ramadhani
MAKUBWA! Dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo amekubali kuruhusu mtoto aliyezaa na mwigizaji Aunt Ezekiel achukuliwe na mume wa mwigizaji huyo, Sunday Demonte aliyeko jijini Abu Dhabi akitumikia kifungo cha msala wa madawa ya kulevya.

Dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo akiwa na mzazi mwenzie  Aunt Ezekiel.
Iyobo ametoa kauli hiyo mara baada ya Sunday ambaye imeelezwa kuwa anaweza kutoka wakati wowote kutokana na utii wake gerezani, kutuma salamu kuwa anafahamu Aunt amezaa na Moze lakini watambue kuwa mtoto huyo ni wake kwani kitanda hakizai haramu.
“Ameweka wazi kabisa kuwa kitanda hakizai haramu hivyo Cookie (mtoto wa Aunt) hawezi kuwafanya watengane, atamchukulia kama mwanaye wa kumzaa kwa kumpa matunzo yanayostahili,” kilisema chanzo.
Alipoulizwa Moze kuhusiana na ishu hiyo, alijibu kwa kifupi: “Kama suala ni mtoto haina shida nitamuachia tu kwani si atapatikana mwingine, siyo ishu sana.”

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

IYOBO AKUBALI KUMUACHIA MTOTO MUME WA AUNT Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin