Friday, 2 October 2015

FAIZA AMBANIA SUGU ‘BETHIDEI’ YA MWANAYE

Msanii ambaye ni mpenzi wa zamani wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally juzikati alimfanyia mwanaye Sasha pati katika siku yake ya kuzaliwa lakini cha ajabu hakumualika mzazi mwezake huyo.

Msanii ambaye ni mpenzi wa zamani wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally akiwa na mwanaye.
Pati hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa Faiza, Mkwajuni jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali ila Sugu hakuonekana eneo hilo.Baada ya kuiona hali hiyo, mwandishi wetu alimuuliza Faiza sababu za Sugu kutokuwepo kwenye siku hiyo muhimu ya mtoto wao ambapo alisema:
“Unajua yule ni baba halali wa mtoto huyu na katika hali ya kawaida alitakiwa kumtakia hata heri ya kuzaliwa lakini hakufanya hivyo. Nahisi hata hakuwa anakumbuka siku hiyo muhimu ya kuzaliwa mtoto wake sasa mimi nisingeweza kumualika kwa sababu bila yeye maisha yanaendelea.”

<<NEXT 1>> 

 <<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

FAIZA AMBANIA SUGU ‘BETHIDEI’ YA MWANAYE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin