Tuesday, 1 September 2015

WANAWAKE WENGI WASOMI AU WENYE KIPATO KIZURI HAWADUMU KWENYE MAHUSIANO..UNA MAONI GANI?


Wadau leo nimeona tujadili hili suala ambalo watu wengi sana mitaani wamekuwa wakiamini hivyo kuwa wanawake wenye kipato kizuri ama wale walio na elimu nzuri, hasa wenye digrii ama zaidi ni vigumu sana kudumu katika ndoa ama mahusiano. 

Na katika mahusiano yao huwa ni yenye migogoro mingi na mivutano sana kwa wenzi wao (Boyfriends ama Waumezao). Humu  wapo kidada wasomi wengi tu ambao wanaweza ”ku-share” uzoefu wao ama kutoa mtazamo wao katika hili. Kina Kaka pia mnaweza kutoa hoja na mitazamo yenu kuhusu hili kwani mahusiano yanahusu pande zote mbili

Ningependa watu tuchangie tukizingatia hasa maswali yafuatayo...

Je, unamaani kuwa huo mtazamo uliojengeka katika jamii una ukweli wowote?

Na kama ni kweli unafikiri nini hasa ndio chanzo?

Na kama unafikiri hii kitu haina ukweli wowote unafikiri ni kwanini basi kuna watu wanaona hivyo?

Mwisho toa ushauri wako kwa kidada wali kwenye kundi hilo ama kina Kaka walio nao katika mahusiano kuhakikisha mambo yanakwenda kama wengine tu.

NB: 
Kumbuka kuwa simaanishi wasichana wote walio katika kundi hilo bali ni walio wengi wao.

<<<NEXT 1>>>

<<<NEXT 2>>>

<<<NEXT 3>>>

<<<NEXT 4>>>

<<<<NEXT 5>>

<<<NEXT 6>>>

WANAWAKE WENGI WASOMI AU WENYE KIPATO KIZURI HAWADUMU KWENYE MAHUSIANO..UNA MAONI GANI? Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin