Thursday, 24 September 2015

MGEJE AMPA MAKAVU MAGUFULI ASEMA ANAFAA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLYMPIC NA SIO KUWA RAISAliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja  ambaye  alijiondoa  na  kuhamia  Vyama pinzani, amesema anashangaa kuona mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, akipiga push up, hivyo akasema anafaa kushiriki michezo ya Olympic na siyo kuwa rais.

Mgeja aliitoa  kauli  hiyo jana  wakati wa mkutano wa kampeni za Lowassa uliofanyika katika ngome ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, Jimbo la Mtama  
 
Alisema mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, Nape anamfahamu na hajawahi kushinda uchaguzi wowote.

"Mna bahati mbaya sana hapa Mtama, sisi tunamwita .... amekumbuka shuka (kwao) wakati kumekucha," alisema na kuongeza Nape siyo mkazi wa Mtama na anakuja jimboni humo akiwa na brief case na kulala nyumba ya wageni kuomba kura.

Akimjibu Mzee John Malecela, aliyesema waliotoka CCM wana matatizo, Mgeja alisema waliotoka CCM ni watu safi.

"Sisi tuliotoka CCM ni watu safi kabisa, ukiwa mchafu CCM huwezi kutoka," alisema.

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

MGEJE AMPA MAKAVU MAGUFULI ASEMA ANAFAA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLYMPIC NA SIO KUWA RAIS Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin