Friday, 25 September 2015

Licha ya Mainda Kudaiwa Kuokoka, Nguo Fupi zaendelea Kumtesa


RUTH Suka ‘Mainda’ aliye msanii wa filamu Bongo ambaye kwa sasa amejikita katika kumtumikia Mungu, amesema mtihani mkubwa ambao bado unampa wakati mgumu katika maisha ya ulokole ni uvaaji wa nguo fupi!

‘Akibadilishana sentensi’ na Amani, Mainda alisema amejitahidi kuruka na kuvuka viunzi vingi tangu kuokoka kwake, lakini ameshindwa kukabiliana na mtihani wa kuachana na uvaaji wa nguo fupi, jambo ambalo anapigana nalo kwa nguvu zote.

“Maisha ya wokovu ni mtihani mno, hakuna ulokole unaopatikana kwa njia rahisi, majaribu ni mengi, kwa mfano mimi uvaaji wa nguo fupi umekuwa mtihani mgumu kuachana nao ingawa kwa sasa najitahidi sana tofauti na zamani, namuomba Mungu anisaidie juu ya hili,” alisema Mainda.

<<NEXT 1>>

<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>

<<NEXT 4>>  

<<NEXT 5>>

<<NEXT 6>>

Licha ya Mainda Kudaiwa Kuokoka, Nguo Fupi zaendelea Kumtesa Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin