Friday, 11 September 2015

BARACKA DE PRINCE AJITENGA NA MASOGANGE


agnesmasogangegerald1.jpgBoniphace Ngumije
Msanii wa muziki, Baracka Endrew ‘Baracka De Prince’ amefunguka kuwa kufuatia skendo iliyokuwa inamkabili ya kutoka kimahaba na Video Queen maarufu Afrika, Agness Gerald ‘Masogange’ ameamua kujiweka naye kando mdogomdogo ili kuepusha maneno kutoka kwa wambeya.
Akichonga na Ijumaa juzikati, Baracka alisema anajua watu wanahisi ‘anabanjuka’ na ‘mtoto’ huyo kutokana na ukaribu wao hivyo ameona ni vyema afanye liwezekanalo ili kuondoa mawazo hayo kwa watu.
“Kiukweli yule wala siyo demu wangu na kwa kuwa huwa sipendi manenomaneno yasiyokuwa na ukweli, nimeamua kupunguza ukaribu na Masogange na hata picha zake nyingi Instargram nimefuta na yeye nilimwambia afanye hivyo akakubali,” alisema Baracka.

BARACKA DE PRINCE AJITENGA NA MASOGANGE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin