Monday, 17 August 2015

OMG!! MWANAMKE ANYOFOLEWA TITI NA KUTAFUNWA,KISA NA MKASA SOMA HAPA

MORO TITI (2)Halima Abdallah, anayedaiwa kucharangwa na mmewe.
Dustan Shekidele, Moro
My God! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Nigar, mkazi wa Kijiji cha Kinole, Morogoro Vijijini anadaiwa kumcharanga mapanga mkewe, Halima Abdallah (28) na kummyofoa titi kisha kulitafuna na kumgeukia mwanaye Tausi (3) na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.
Tukio hilo lililomfanya mwanahabari wetu kufunga safari hadi kijijini hapo lilijiri Agosti 14, mwaka huu ambapo mwanaume huyo alikuwa kwenye shamba lao la migomba ndipo alipotekeleza unyama huo kabla ya kukamatwa na kufikishwa polisi.
MORO TITI (1)Wakizungumza na gazeti hili kijijini hapo, mashuhuda wa tukio hilo, Msimbe Joseph na Mchilo Agustino walisikitishwa na tukio hilo na kwamba hawakujua nini kilimpata baba Tausi hadi kufikia uamuzi huo.Baada ya kutoka kijijini hapo, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Halima akiwa wodi namba 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa sharti la kutomwambia kama mwanaye Tausi alikuwa amechinjwa na baba yake kwani hakujua kilichoendelea kijijini hapo baada ya kucharangwa na kuwa hoi.
kamanda leonard paulKamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
Alisimulia kwa masikitiko: “Nimeishi na mume wangu kwa zaidi ya miaka 10, tumebahatika kupata watoto wawili. Siku ya tukio, nakumbuka ilikuwa saa 8:00 usiku, mume wangu alikurupuka kitandani na kudai kuwa aliota ndoto ya ajabu.
“Aliondoka nyumbani usiku huo na kwenda kulala msikitini. Aliporejea asubuhi alichukua panga akasema twende kwenye shamba letu la migomba.
“Tulipofika huko ndipo alipoanza kunishambulia kwa kunikata sehemu mbalimbali mwilini.
“Kama hiyo haitoshi, alinirukia akaning’ata titi la kushoto hadi akalinyofoa na kuanza kulitafuna kama nyama na kumeza.
“Baada ya hapo niliokolewa na wanakijiji wakanipeleka zahanati ya kijiji ndipo nikahamishiwa hapa (Hospitali ya Morogoro).
“Bado hali yangu si nzuri kwani nasikia maumivu makali. Nasikia baba Tausi alikamatwa anasubiri kufikishwa mahakamani.”Kwa upande wao ndugu na wanakijiji wenzao waliendelea na mazishi ya mtoto Tausi huku mama yake akiwa hajui kama mwanaye alipatwa na umauti.
Gazeti hili lilipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul alisema hajalipata tukio hilo lakini alimwagiza msaidizi wake kulifuatilia na kupata ripoti kamili juu ya tukio hilo.

<<<NEXT 1>>>

<<<NEXT 2>>>

<<<NEXT 3>>>

<<<NEXT 4>>>

<<<<NEXT 5>>

<<<<NEXT 6>>

OMG!! MWANAMKE ANYOFOLEWA TITI NA KUTAFUNWA,KISA NA MKASA SOMA HAPA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin