Wednesday, 19 August 2015

KWA STAILI HII HAPA LAZIMA KUUGUA KIPINDUPINDU

OFM (3)


Wandishi Wetu
INATISHA! Hivi ndivyo unavyoweza kusema mara tu unapofika katika hospitali ya serikali ya Kijitonyama, iliyopo Sinza Mapambano jijini Dar es Salaam kwani kuna uchafu mwingi unaoenda tofauti kabisa na mazingira yanayostahili katika kituo hicho cha huduma za afya, Risasi Mchanganyiko linakuthibitishia.
OFM (2)

Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, juzikati kilitinga katika…..zahanati hiyo kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya wagonjwa juu ya kutoridhishwa na usafi, hasa maeneo muhimu ya kujisaidia haja ndogo na kubwa.
OFM ilishuhudia vyumba vya vyoo vikiwa gizani, matundu matatu ya vyoo hivyo yakiwa yameharibika vibaya kwa uchakavu na mbaya zaidi, kutokuwepo na maji ya kutosha.
Baadhi ya wagonjwa waliwaambia OFM kuwa wanawake ndiyo wako kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi, kwa sababu ya uchafu uliokithiri huko, kwani upo uwezekano mkubwa wa mtu kuondoka na ugonjwa mwingine licha ya uliompeleka katika zahanati hiyo.
OFM (5)

Makamanda wetu waliingia kazini mara moja na kubaini ukweli kuwa mazingira ya zahanati hiyo hayazingatii usafi, kwani katika eneo la mapokezi, walishuhudia uchafu wa damu sakafuni na vipande vipande vya pamba vikiwa vimezagaa chini huku wauguzi wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kama kawaida.
Katika vyumba vya vyoo, licha ya kuwa na giza, kulikuwa na uchafu mwingi unaomzuia mgonjwa kuingia ndani hivyo kuwaweka katika hali ngumu wale wanaohitaji kupima haja ndogo na kubwa kabla ya kupatiwa matibabu.
OFM-(1)

Aidha kwa upande wa maji, pia ni tatizo kubwa kwani matundu yote matatu yanategemea ndoo moja tu iliyopo nje ya vyoo hivyo hali ambayo pia inaweza kusababisha maambukizi kwa wagonjwa.
Akizungumzia hali hiyo, Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Lazarius Mhojah, alikiri kuwepo kwa mazingira hayo machafu, lakini akajitetea kuwa uongozi wao una muda mfupi tangu uanze kazi.
OFM-(4)

OFM (1)1

Ni kweli hali siyo nzuri, lakini siyo upande wa maji tu, bali huduma zote. Hii inatokana na wingi wa wagonjwa na udogo wa vifaa na huduma, watu ni wengi kuliko uwezo wa zahanati yenyewe. Hata hivyo, hivi karibuni Kamati ya afya inatarajiwa kukaa kujadiliana kuhusu mazingira ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya matundu ya vyoo,î alisema.

<<<NEXT 1>>>

<<<<NEXT 2>>

<<<<NEXT 3>>

<<<<NEXT 4>>

<<<<NEXT 5>>

><<<NEXT 6>>

KWA STAILI HII HAPA LAZIMA KUUGUA KIPINDUPINDU Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin