Monday, 24 August 2015

JOKETI A.K.A KIDOTI NA ALI KIBA SASA MAHABA NJE NJE!! WAKENYA WABAKI NA MSHANGAO

jokate ali kiba
Mtoto mzuri Jokate Mwegelo akiwa na staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
Musa Mteja
MAHABA nigaragaze! Mtoto mzuri Jokate Mwegelo na staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba wameoneshana mahaba hadharani nchini Kenya.
Ishu hiyo ilijiri juzikati wakati Kiba alipokwenda kwenye ‘project’ ya Coke Studio inayoshirikisha wasanii mbalimbali duniani kurekodi nyimbo za pamoja, ndipo wawili hao walipotumia mwanya huo kufanya yao.
jokate
Mtoto mzuri Jokate Mwegelo.
Kwa mujibu wa chanzo kilichokuwepo nchini humo, wasanii hao walikuwa gumzo kwani walionesha mahaba kila mahali walipokwenda kuanzia hotelini na studio.
“Daah yaani kama Bongo huwa wanafichaficha, huku wamefanya laivu. Nahisi wameona kwa huku hakuna watu wa kuwafuatilia kivile halafu si unajua hawa ni watu wa sirisiri sana.
“Walifikia kwenye hoteli moja na mimi kuna muda nilimshuhudia Kiba akimtambulisha Jokate kuwa ni mkewe kwa msanii mmoja wa Kundi la Sauti Soul.
Jitihada za kumpata Kiba ili kutia neno kuhusiana na kujiachia huko hadharani tofauti na wanavyokuwa Bongo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa.

<<<NEXT 1>>

<<<NEXT 2>>

<<NEXT 3>>>

<<<NEXT 4>>

<<<NEXT 5>>

<<<NEXT 6>>

JOKETI A.K.A KIDOTI NA ALI KIBA SASA MAHABA NJE NJE!! WAKENYA WABAKI NA MSHANGAO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin