Friday, 14 August 2015

HUYU NDIYE MDOSI ALIYEPORWA DEMU WAKE PAMOJA NA KUWA NA PESA NYINGI SANA

MDOSI (1)
Ramesh mwenye asili ya kiasia (Mdosi), anayedaiwa kupora mke wa mtu.
Gladness Mallya na Hamida Hassan
Jamaa mmoja anayefanya kazi kwenye kiwanda kimoja cha plastiki jijini Dar aliyejulikana kwa jina moja la Ramesh mwenye asili ya kiasia (Mdosi), anadaiwa kumpora mke wa mtu na kuishi naye kinyumba na kuiacha ndoa yao ikiyumba, Ijumaa lina ushahidi.
MDOSI (2)Shufaa Adam, mke wa mtu anayedaiwa kuporwa na mdosi.
Mume wa mke aliyeporwa, Mashaka Ali, mkazi wa Vingunguti jijini Dar aliliambia gazeti hili kuwa alifunga ndoa na Shufaa Adam mwaka 2004 na katika maisha yao wamejaaliwa kupata watoto wawili, ambao bado ni wadogo kwa sasa.
Alisema baada ya kuanza kuishi katika ndoa, alimtafutia mkewe kazi katika kiwanda hicho, lakini mapema mwaka huu, mwanamke huyo alianza kuonesha mabadiliko yaliyompa wasiwasi na hivyo kufanya uchunguzi uliomfahamisha kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mdosi huyo.
 “Niliamua kwenda kuripoti polisi, mwanaume aliitwa na kukiri kwamba ni kweli ana uhusiano na mke wangu na akaandika barua kwamba hatarudia tena lakini hakuna kilichobadilika.
“Kila Jumapili mke wangu akawa anatoka nyumbani bila kuniaga ambapo nilimfuatilia siku moja na kumuona akipanda kwenye gari la huyo Mdosi, nilimfuatilia kwa bodaboda mpaka hotelini, nikaamini nilichoambiwa.
“Nilipokuja kumuuliza mke wangu akaja juu na akaamua kuondoka kabisa nyumbani, akaenda kupangiwa nyumba na huyo mwanaume akiwaacha watoto, ukweli nateseka sana, nimeenda mpaka ustawi wa jamii lakini hakuna kilichoeleweka mpaka sasa imepita miezi sita,” alidai Mashaka.
Gazeti hili lilimtafuta mdosi huyo aliyekanusha habari hizo, akimwita Mashaka kuwa ni mtu asiye na akili na kwamba anakwenda kumshtaki polisi, lakini wakati huo huo akiomba kuja ofisini kwetu kwa mazungumzo (Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni hakufika, jitihada za kuzungumza naye zinaendelea.)
Kwa upande wake, mke wa Mashaka, Shufaa alipotafutwa, alikana kukimbia ndoa yao kwa sababu ya mwanaume mwingine, bali kuchoka vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mumewe.
“Suala la mdosi siwezi kuliongelea lakini nimeondoka kwenye ndoa kwa sababu ya kupigwa na mume wangu, sasa nashangaa ananing’ang’ania nini,” alisema Shufaa na kudai kuwa watoto wake humtembelea mara kwa mara anapoishi.

<<<NEXT 1>>>

<<<NEXT 2>>>

<<<<NEXT 3>>>

<<<<NEXT 4>>>

<<<<NEXT 5>>>

<<<NEXT 6>>>

HUYU NDIYE MDOSI ALIYEPORWA DEMU WAKE PAMOJA NA KUWA NA PESA NYINGI SANA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin