Wednesday, 19 August 2015

HEE!! SHILOLE,AUNT WAJISHEBEDUA NA VISERENGETI BOY VYAO MBELA YA JK


JK (1)
Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na rais wa Shilikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba.
Waandishi Wetu
ISHU! Katika kitu kinachoweza kutafsiriwa kama kituko, wasanii wawili wanaofanya vizuri kwenye filamu na Bongo Fleva, Aunt Ezekiel na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ juzikati walionekana wakijishebedua na wapenzi wao wanaotajwa kuwa ‘majanki’ kuliko wao, mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya fainali ya Kinondoni Talent Search, iliyofanyika katika ukumbi wa Kisanga, Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
NUH SHILOLEZuwena Mohamed ‘Shilole’ na mpenzi wake, Nuh Mziwanda.
Wawili hao walitinga ukumbini hapo wakiwa na wapenzi wao hao na kukaa pamoja huku wakipigana vibega kama ilivyo kawaida ya wapenzi, kiasi cha kuwaacha watu midomo wazi, hasa kwa kuzingatia kuwa ndani ya ukumbi huo kulikuwa na ugeni mkubwa.
AUNT IYOBOAunt Ezekiel na mpenzi wake, Mose Iyobo.
Wakiwa kwenye fainali hizo zilizoratibiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Aunt na Shilole muda mwingi walionekana wakichezacheza na mabwana zao hao, Mose Iyobo na Nuh Mziwanda.
“Dah angalia Shilole na Nuh wake wanavyojishebedua mbele ya JK utadhania wao ndiyo wageni rasmi vile, halafu hali hiyo pia nimeiona kwa Aunt na Mose Iyobo na wao wamekaa kule nyuma lakini muda wote ni kunong’onezana na kucheka tu na hawaachani utafikiri wamekuja kutangaza mapenzi na ndoa zao humu,” alisema mmoja wa mashuhuda.

<<<NEXT 1>>>

<<<<NEXT 2>>

<<<<NEXT 3>>

<<<<NEXT 4>>

<<<<NEXT 5>>

><<<NEXT 6>>

HEE!! SHILOLE,AUNT WAJISHEBEDUA NA VISERENGETI BOY VYAO MBELA YA JK Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin