Thursday, 16 July 2015

AUNT EZEKIEL AELEZA SABABU YA KUMFICHA MWANAYE

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Mama Cookie la Princessa’.
MSANII wa filamu ambaye amejipatia hadhi ya kuitwa mama baada ya kujifungua motto wa kike aliyempa jina la Cookie la Princessa, Aunt Ezekiel, amefunguka sababu ya kumficha sura mwanaye ambaye tangu amezaliwa sura yake hajaiweka wazi.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Aunt alisema kuwa sababu kuu ya kumficha sura mwanaye ni kuepuka watu wanaomiliki vibaya mitandao ambao huweza kumchafua mtu wanavyotaka na kuongeza kuwa hayupo tayari kuona mwanaye akichafuka katika umri mdogo.
“Siwezi kumuonesha kwa sasa kwa sababu kuna watu watamchafua mitandaoni na kusema wanavyovitaka, muda ukifika nitamwonesha,” alisema Aunt ambaye muda mchache baada ya kuzungumza na paparazi wetu aliweka picha ya mtoto mtandaoni akidai kuwa ni mwanaye Cookie lakini alipingwa vikali na mashabiki wake waliodai kuwa mtoto huyo siyo wake kwa kuwa ni mkubwa.

AUNT EZEKIEL AELEZA SABABU YA KUMFICHA MWANAYE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin