Tuesday, 2 June 2015

OMMY DIMPOZ AKANUSHA MAHUSIANO NA WEMA

Star wa Bongo Flava anayeiwakilisha vema Kigoma Omary “Dimpoz” Faraja “Ommy dimpoz”, amesema hana na wala hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Wema Sepetu.

Akichezesha “taya” na ripota wa www.timesfm.co.tz juzi kati, mkali huyo amedai uhusiano wake na Wema ulikuwa ni kwenye video tu ya Wanjera lakini si nje ya hapo.

“Kila Biashara ina promo yake, na ile ilikuwa promo yetu kwa ajili ya biashara umeelewa eeh na naweza sema kama ime work out kama tulivyotarajia, tulitengeneza tu na wema sisi ni washikaji” amesema Dimpoz.

Dimpoz ametusanua pia maendeleo ya Video yake ya “Wanjera”, kwa kusema imepokelewa vizuri Africa kwa kuchezwa na Televison mbali mbali.

OMMY DIMPOZ AKANUSHA MAHUSIANO NA WEMA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin