Saturday, 13 June 2015

MWIGIZAJI LULU ATOBOA SIRI YA KUTOFANYA 'MOVE' KWA MWAKA MZIMA

Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael,’Lulu’amefunguka sababu ya kutofanya filamu kwa mwaka mzima kuwa alikuwa bize na shughuli zingine ikiwemo masomo.

Akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa mwaka jana wote alikuwa ‘host’ kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya uigizaji (Tanzania Movie Talents) ambayo ilifanyika karibu mikoa yote,pia alikuwa bize na masomo katika chuo cha  Magogoni akichukua kozi ya Public Administration.

‘’Mwaka jana wote sikufanya filamu kabisa kutokana na kuwa bize kwenye shindano la kutafuta vipaji vya uigizaji na pia shule nayo ilinibana kwahiyo sikuwa na muda wa kufanya filamu,’alisema Lulu.

MWIGIZAJI LULU ATOBOA SIRI YA KUTOFANYA 'MOVE' KWA MWAKA MZIMA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin