Wednesday, 3 June 2015

MAREHEMU RECHO HAULE ADAIWA KUMTOKEA MUMEWE UPYA, MAUZA UZA YOTE YAKO HAPA


GEORGE Saguda ambaye mchumba wake, marehemu Rachel Haule ‘Recho’ wiki iliyopita alitimiza mwaka mmoja kaburini, anadai kutokewa na mzimu wake ukimueleza mambo mbalimbali hasa akiwa katika wakati mgumu.
Marehemu Rachel Haule ‘Recho’.
Akipiga stori na gazeti hili, Saguda alisema tangu alipofariki mchumba wake amekuwa akiishi kwa mateso kwani amejaribu kuwa na mwanamke mwingine ili kupoteza mawazo lakini imeshindikana.
George Saguda akiwa na aliyekuwa mchumba wake marehemu Sheila Haule ‘Recho’.
“Mzimu wa Recho hivi sasa unanitokea mara kwa mara hasa nikiwa kwenye wakati mgumu, anakuja na kunielekeza jinsi ya kufanya ili kulitatua tatizo husika ambapo kweli huyafuata na kujikuta nikiwa fresh,” alisema Saguda.

MAREHEMU RECHO HAULE ADAIWA KUMTOKEA MUMEWE UPYA, MAUZA UZA YOTE YAKO HAPA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin