Friday, 19 June 2015

MAHABA NIUWE ZARI AMPA DIAMOND GARI LA MIL.500


MAMA kijacho wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amewadhihirishia mashabiki wa bwana’ke huyo kuwa yuko fiti kifedha kwa kumpatia gari aina ya Ferrari 548 Spider lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 500.

******CLICK NEXT*****


Mama kijacho wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
TUJIUNGE SAUZI
Kwa mujibu wa mmoja wa Timu ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond, tukio hilo lilijiri mapema wiki hii nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ mara tu baada ya mkali huyo wa Ngoma ya Nana ‘kupafomu’ kwenye shoo ya kutajwa kwa majina ya wanaowania Tuzo za MTV Base (MAMA’S).
Mbali na shoo hizo, pia ilifahamika kwamba, Diamond yupo Sauzi kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya video na nyimbo zake ambazo alizifanya na kulikuwa na mambo madogomadogo hayajakamilika.
ZARI WA MAGARI
‘Ubuyu’ zaidi ulidai kwamba, Zari aliamua kumpa mkoko huo wa bei mbaya kwani mwanadada huyo ana magari mengine kibao ya kifahari hivyo kutoa ‘hako kamoja’ si ishu kwake.
Gari anayodaiwa kununuliwa Diamond Platnumz na mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
BOFYA HAPA KUMSOMA DIAMOND
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilizungumza moja kwa moja na Diamond akiwa nchini humo ambapo alifunguka kuwa, kweli anajivunia kwa sasa kuwa na mwanamke mwenye upendo wa hali ya juu kiasi hicho, kwa kuweza kuendelea kumsapoti katika kila hatua ya maisha yake.
Diamond alifunguka kuwa moja ya sapoti kubwa ni suala hilo la kumpatia gari lenye gharama kubwa kwa ajili ya kufanyia kazi zake za kimuziki anapokuwa Sauzi akianza kulitumia kwenye kutengeneza video za Yamoto Band ambao yupo nao nchini humo.
AMMWAGIA SHUKURANI
“Nina faraja kubwa moyoni mwangu kwani hadi sasa naamimi kabisa nipo katika mikono salama kwa huyu mwanamke.
“Namshukuru sana Zari, ni mtu ambaye amekuwa akitamani kila ninachokifanya walau naye aoneshe mchango wake hata kama si lazima. “Kwangu ni jambo la kipekee sana kuona mtu anajitolea gari ya gharama kubwa kama hili.”
SAPOTI YA NGUVU
“Nimekuwa nikipata tabu sana katika video zangu nyingi kupata magari ya hadhi kubwa kwa ajili ya kufanyia video, lakini hali hii kwa sasa naona kama inaenda kupotea kufuatia mpenzi wangu kuwa bega kwa bega katika kunisapoti.
“Ninaamini ni wanawake wachache sana wanaoweza kufanya haya, maana nipo kwenye ‘game’ muda sasa na nimeshapata uzoefu mkubwa juu ya usumbufu wa vitu hivi.”
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
“Gari hili nimeletewa na ndugu yake Zari na nimeanza kufanya nalo video za Yamoto Band ambao nimejitolea kuwasapoti ili tu muziki wetu upenye zaidi katika anga za kimataifa maana mwenendo wao pia si mbaya na wana moyo wa kufika mbali.
HAKUNA KAMA ZARI
“Imefikia kipindi sasa naweza kusema kwangu hakuna mwanamke kama Zari, maana vitu anavyonifanyia kila kukicha vinaonesha mwanga wa kunivusha kwenye maisha magumu na kunipeleka kwenye mafanikio makubwa ambayo nimekuwa nikiyatamani kwa muda mrefu.
“Ninasema hivi kwa kuwa nimekuwa nikijionea mengi kutoka kwake na amekuwa na shauku ya kufanya na mimi mambo makubwa kila kukicha,” alisema Diamond.Kwa sasa Diamond anasubiri kupata mgeni katika familia yake kwani kitumbo cha Zari kinazidi kukua kila kukicha.


BONYEZA HAPA KUPATA UBUYU>>> ****CLICK HERE****

MAHABA NIUWE ZARI AMPA DIAMOND GARI LA MIL.500 Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin