Saturday, 13 June 2015

LICHA YA KUJIFUNGUA UZURI WA AUNT PALEPALE

MWANDISHI WETU
KIWANGO! Tofauti na watu wengine ambao maumbile yao hubadilika mara baada ya kujifungua, kwa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel hali imekuwa tofauti, uzuri na umbo lake limebaki vilevile.

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa na mwanaye.
Akizungumza na wahariri sambamba na waandishi wa Global Publishers nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kilichomfanya asinenepe kupita kiasi na kuharibika mwili ni mazoezi sambamba na kufuata ushauri wa vyakula anaopewa hivyo mwili wake kubaki vilevile.
“Nachukia ubonge nyanya, namshukuru Mungu pia kwani wengi wakijifungua huwa wananenepa hovyo lakini kwangu mambo yamekuwa tofauti. Niko vilevile, nafikiri pia ni kutokana na kufuata ushauri mzuri wa kula chakula niliopewa,” alisema Aunt.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Mbali na kutobadilika, Aunt alisema kwa sasa muda mwingi anautumia kuwa nyumbani na ubavu wake, Moze Iyobo wakimlea mtoto wao tofauti na zamani alipokuwa na misele ya usiku katika viwanja tofauti vya starehe.

LICHA YA KUJIFUNGUA UZURI WA AUNT PALEPALE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin