Friday, 29 May 2015

WACHINA 15 MBARONI KWA KUGUSHI VYETI

Wanafunzi raia wa China wanaosoma katika Chuo Kikuu cha New York nchini Mrekani.
Raia wa China wakiwa 'kortini'.
Raia 15 wa China wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka nchini Marekani kwa tuhuma za udanganyifu wa matokeo ya elimu zao na kugushi nyaraka za kitaaluma walizozitumia wakati wakijiunga na elimu ya juu nchini Marekani.
Kwa mjibu wa waendesha mashtaka nchini marekani, wamebaini kuwa vijana hao wa China wamekuwa wakifanya udanganyifu huo kwa kutumia simu za kiganjani wakati wa majaribio ya kujiunga na vyuo hivyo.
Idara ya sheria nchini Marekani imesema kuwa, kwa kipindi cha miaka minne iliyopita Wachina hao wamekuwa wakikwepa mfumo halali wa uchaguzi wa majina ya vyuo wa nchini Marekani na badala yake kutumia majina bandia (yasiyo yao) na pasi za kusafiria.
Idara hiyo imeongeza kuwa, iwapo raia hao watakutwa na hatia kutokana na tuhuma hizo, watafungwa hadi miaka 20 jela.

WACHINA 15 MBARONI KWA KUGUSHI VYETI Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin