Thursday, 28 May 2015

UKATILI WA KUTISHA..!! MTOTO ALAWITIWA NA KUUAWA KISHA KUNYOFOLEWA KORODANI ZAKE NA ULIMI HUKO ROMBO, KILIMANJARO

Mtoto Fraterin Massawe (11) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Magereza aliokotwa akiwa ametupwa katika shamba linalomilikiwa na masista wa kanisa katoliki lililopo Karanga manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Tukio limetokea Mei 23, mwaka huu saa 1:00 asubuhi katika kijiji cha Katanini kata ya Karanga manispaa ya Moshi.
Mtoto huyo amekutwa akiwa na jeraha kubwa usoni, huku korodani zikiwa zimeondolewa pamoja na ulimi na kwamba anaonekana kulawitiwa kutokana na kukutwa na haja kubwa .

Taarifa za awali zinasema mtoto huyo alitoweka nyumbani Mei 21, mwaka huu na kwamba alionekana na mtu alitajwa kuwa ni Mariki Peter Olomi (45) mkazi wa Kibosho road.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Flugence Ngonyani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi na mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.

UKATILI WA KUTISHA..!! MTOTO ALAWITIWA NA KUUAWA KISHA KUNYOFOLEWA KORODANI ZAKE NA ULIMI HUKO ROMBO, KILIMANJARO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin