Monday, 25 May 2015

UBONGO WA KAJALA WAPATA TATIZO?, DAMU YAGANDA! HABARI KAMILI IPO HAPA...

Kajala Masanja akionekana na jeraha usoni kipindi ambacho alikua amepigwa chupa. Maskini Kajala! Ndivyo unavyoweza kusema ukisikia mkasa wa staa wa kiwango cha juu kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, ambaye anadaiwa kwa hivi sasa hayuko sawa kiafya baada ya kupigwa chupa kichwani akiwa katika shoo ya kumchangia mke wa msanii Mabeste iliyofanyika New Maisha Club, Masaki jijini Dar.
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala kimeliambia Ijumaa Wikiendakwamba, tangu staa huyo akumbwe na sekeseke hilo amekuwa katika kipindi kigumu kwani amekuwa akipata maumivu makali sehemu ya kichwani huku akianguka mara kwa mara.
Kajala Masanja. Kilidai kwamba, pia Kajala amekuwa akipata kizunguzungu kikali hivyo kujiona yupo kwenye hatari kubwa hasa ikitokea akaanguka vibaya kwani anaweza kupoteza maisha.

UBONGO WA KAJALA WAPATA TATIZO?, DAMU YAGANDA! HABARI KAMILI IPO HAPA... Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin