Monday, 18 May 2015

MUME WA ZARI ANASA KIMAPENZI KWA SHOSTI WA ZARI, NI BAADA YA ZARI NAYE KUHAMIA KWA DIAMOND

Habari kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba aliyekuwa mume wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kunasa penzi la shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo aitwaye Stella Nankya, Ijumaa Wikienda limetonywa.

Aliyekuwa mume wa Zari akiwa na mpenzi wake mpya ambaye ni shosti wa kufa na kuzikana wa Zari.

Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.

Zari akiwa na shosti wake Stella Nankya ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’.


Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.

Modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’ Stella Nankya akiwa katika pozi.


“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti moja la nchini Uganda.

Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.

Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.

Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:

“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”

Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote.

MUME WA ZARI ANASA KIMAPENZI KWA SHOSTI WA ZARI, NI BAADA YA ZARI NAYE KUHAMIA KWA DIAMOND Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin