Friday, 1 May 2015

MKE WA MAFUFU ABEBA VIRAGO!


Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
KIMENUKA! MKEwa staa wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki amenaswa akifungasha virago nyumbani kwake Mwananyamala-Hospitali na kuelekea kwa wazazi wake maeneo ya Mbagala jijini Dar akidai kuchoshwa na tabia za mumewe huyo, Ijumaa lina ‘full’ stori.
Mkewa staa wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki akiwa na mizigo yake.
Akizungumza na mapaparazi wetu, Salma alisema kwa kipindi kirefu msanii huyo amekuwa akimuonyesha tabia za ajabu ikiwemo hivi karibuni kunaswa akiwa amezungukwa na vimwana kana kwamba si mume wa mtu.“Mara nyingi akiwa anatoka kwenye shughuli za usiku huwa tunatoka wote lakini cha ajabu kuna siku alinigomea kabisa kwenda naye kwenye lile onesho la Twanga Pepeta, akarudi saa 11 alfajiri na kwenye bethidei ya mtoto wa Davina akaniambia mimi nibaki nyumbani kumbe alikuwa ana mambo yake huko kwani alirudi asubuhi saa 12.
Siku ya harusi yao.
“Nimevumilia mengi sana kwenye hii ndoa mpaka leo kuamua kuondoka. Acha nimuache na mambo yake,” alisema Salma kwa masikitiko.Alisema japo katika uhusiano wao wana miaka isiyopungua saba, walikuwa kwenye uchumba kwa miaka minne na baadaye wakafunga ndoa mwaka 2013 lakini anashindwa kukumbuka alipotoka.
Baada ya kushuhudia Salma akiondoka nyumbani hapo, mapaparazi wetu walimtafuta Jimmy kwa njia ya simu ili kumsikia anazungumziaje madai ya mkewe ambapo alisema mkewe huyo amekuwa akimuonea wivu usiokuwa na maana.
Mafufu akiwa na warembo.
“Mke wangu nampenda sana na tangu nimuoe sijawahi kumsaliti sema tu anakosa imani kwa mambo madogo sana. Kama mwenyewe kaamua kuondoka kutokana na wivu wake mimi siwezi kumfuata,” alisema Mafufu.

MKE WA MAFUFU ABEBA VIRAGO! Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin