Thursday, 14 May 2015

MASTAA WA MAJUU, KIM AJIVUNIA KANYE WEST KUITWA DOKTA


Mwanamitindo na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian.
Chicago, Marekani
MWANAMITINDO na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian ameonesha furaha sambamba na kujivunia mumewe, Kanye West kutunukiwa shahada ya udaktari wa sanaa (PHD) katika Chuo cha School of Art Institute jijini Chicago.
Kanye West alipotunukiwa shahada hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo aliyekuwepo nchini Brazil akikitangaza kitabu chake kiitwacho Selfish, alishindwa kuhudhuria katika siku ya kutunikiwa mumewe na kuamua kuweka mapenzi yake kwa kuandika;
“Dkt. Kanye West!!!! Najivunia kuwa na wewe mpenzi na najua hata mama yako atakuwa anajivunia kwa hilo.”
Kanye na Kim walioona mwaka 2014 pande za Forte di Belvedere in Florence, Italia.

MASTAA WA MAJUU, KIM AJIVUNIA KANYE WEST KUITWA DOKTA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin