Monday, 18 May 2015

KWELI MAISHA NI SAFARI..!! KUMBE WASANII WENGINE WA KUNDI LA TMK WANAUME SASAIVI NI MAFUNDI FENICHA.


Katika makundi makubwa ya muziki wa kizazi kipya ambayo yamewahi kutajwa Tanzaniana kufanya vizuri ni pamoja na Tmk Wanaume Family ni kundi ambalo lilikuwa na zaidi ya watu 5 swali ni kwamba wengine wako wapi kwa sasa??

Hili ni swali ambalo watu wengi tumekua tukijiuliza hasa baada ya project nyingi kuwasikiaTemba na Chege peke yao,kipaza kinamfikia Said Fella ambaye ni meneja wa kundi laTmk Wanaume Family>>’Unajua wengi wamekua wajasiriamali‘

Hapa anaendelea>>’ Tripo kwa sasa anasimamia na kuuza Fenicha za kaka yake mwingine ni Zozo Wida ambaye yeye kwa sasa amenunua Pikipiki za miguu mitatu ndizo zinazomuingizia kipato‘

Mwingine aliyetajwa ni Sticco ambaye Fella amesema>>’Kwa sasa Sticco ana production ya kutengeneza filamu‘ Fella amesema ingawa kila mtu ana majukumu yake lakini ikitokea wanahitajika wote wanapatikana na kufanya show pamoja.

Tmk Wanaume Family October 20 2014 walimpoteza member mwenzao mmoja anaeitwaYp ambaye alifariki akiwa hospitali ya Temeke,Rest in peace Yp.

KWELI MAISHA NI SAFARI..!! KUMBE WASANII WENGINE WA KUNDI LA TMK WANAUME SASAIVI NI MAFUNDI FENICHA. Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin