Tuesday, 5 May 2015

HII NDIYO SINEMA KAMILI UGAIDI HUKO MOROGORO !

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Wakazi wa Wilaya ya Kilombero mkoani hapa, wametoboa siri ya tukio linaloonesha picha ya ugaidi lililotokea Mei Mosi, mwaka huu huku askari mgambo Thomas Manjole (54) aliyejeruhiwa  na bomu la kurushwa akisimulia mkasa mzima jinsi alivyopambana.

Askari mgambo Thomas Manjole akiwa na majeraha, hospitalini.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni takriban wiki mbili tangu Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kufanikiwa kuzima jaribio la ugaidi kwa kuwakamata watu 10 wakiwa ndani ya Msikiti wa Answari Suni uliopo Wilaya ya Kilombero.
KAWAIDA YA GAZETI LA UWAZI
Baada ya tukio la Mei Mosi, Uwazi lilifunga safari hadi wilayani humo ili kuchimba kwa kina tukio hilo ambalo simulizi yake ni kama sinema.Hali miongoni mwa wananchi ilikuwa bado tete, walisema wanaishi kwa hofu kubwa kufuatia matukio hayo mawili ya ugaidi kutekelezwa ndani ya wilaya yao.
KUMBI ZA STAREHE ZADODA, WATU WAJIFUNGIA
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba, saa 12 jioni baadhi ya watu hujifungia majumbani mwao jambo linalosababisha baa na kumbi za starehe kukosa wateja na kufungwa saa moja usiku.
“Kiukweli tunaishi kwa hofu kubwa  tangu matukio haya mawili ya ugaidi kutokea katika wilaya yetu, watu ikifika saa 12 jioni tunajifungia ndani.”
...Nesi akimuhudumia.
KISASI CHATAJWA
“Mimi na baadhi ya wananchi wenzangu tunahisi hawa magaidi wa juzi wamekuja kulipa kisasi baada ya wale wenzao kumi kukamatwa na mmoja wao kuuawa na wananchini  wenye hasira,” alisema Bi. Ashura Senga.
UWAZI LATINGA HOSPITALI KWA MGAMBO
Baada ya kuzungumza na baadhi ya wananchi, gazeti hili lilifunga safari hadi Hospitali ya Mtakatifu Kizito, Mikumi na kufanikiwa kufanya mahojiano maalum na majeruhi wa tukio hilo, akiwemo askari mgambo Manjole.
Akisimulia mkasa mzima lakini kwa shida huku akiwa wadi namba tatu hospitalini hapo, mgambo huyo alisema:
”Siku ya tukio, majira ya usiku nilikwenda kwenye kibanda cha simu kuchukua simu yangu ambayo niliiacha ikichajiwa. Nikiwa pale, alinifuata Mwenyekiti wa Kitongoji cha ltefa,  anaitwa Joseph Mhanga akiwa na watu wawili.
“Aliniambia kwamba watu hao ni wageni kwenye kitongoji chetu na kwamba alivyowahoji hakukubaliana na maelezo yao hivyo akaniomba tuwachukue hadi kwenye ofisi ya kata.
“Lakini kabla ya kufika huko tulipata taarifa kuwa, karibu viongozi wote wako kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Mei Mosi iliyofanyika kwenye Ofisi ya CCM, tukaenda kwenye ofisi hiyo na watuhumiwa wetu.”
MGAMBO ATAKIWA KUWASACHI
“Diwani wa Kata ya Sanje, Daudi Ligosio ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero tulipomsimulia kuhusu watu hao, aliniamuru kuwapekua watu hao ambao hawakuwa na mabegi.
”Basi, mimi kwa kushirikiana na watu wawili, Amos  Msopolena na Novatus  Ngope nilianza kuwapekua mifukoni watuhumiwa hao. Mtuhumiwa wa kwanza ambaye hajui Kiswahili nilipompekua mifukoni nilimkuta ana viberiti vitatu vya gesi, laini ya simu na shilingi elfu 10.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamanda SACP Leonard Paul akionyesha baadhi ya zana hizo.
“Wa pili ambaye anajua Kiswahili vizuri aliyejitambulisha kwa jina la lssa Abubakar, cha ajabu kabla ya kuanza kumpekua mifukoni alitoa kitabu cha dini, kichupa chenye maji na tochi yenye mwanga mkali.
AGOMA KUSACHIWA, ACHEZA KARETI
”Tulimsachi mfuko wa kwanza, akatulia, cha ajabu nilipotaka kumsachi mfuko wa pili wa kulia aligoma. Nikahangaishana naye sana, ndipo wenzangu watatu wakaungana nami kutumia nguvu.
“Tulipoanza kumshinda, ndipo akaturukia kwa sarakasi huku akicheza kareti na kufanikiwa kutusambaratisha wote tukaanguka.

Mfano wa bomu.
“Baada ya kuona hivyo watu waliongezeka na kumdhibiti ndipo alipozidiwa nguvu alitoa bomu kwenye ule mfuko aliogoma kusachiwa na kuturushia na kutujeruhi kama hivi.”Watu waliojeruhiwa na bomu hilo ni Novatus Ngope ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero anayeendesha gari lenye namba za usajili SM 10632, mgambo huyo ambaye hali yake ni mbaya na jana (Jumatatu) alitarajiwa kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mwingine ni Amos Msopole, Azama  Naniyunya na Anna Pius.
Baada ya kutenda uhalifu huo, watuhumiwa wote wawili walifanikiwa kutoroka.
Wakati mwandishi wetu akirejea Morogoro mjini akitokea Kilombero alikutana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamanda SACP Leonard Paul katikati ya Mbuga ya Wanyama ya Mikumi akielekea eneo la tukio.

HII NDIYO SINEMA KAMILI UGAIDI HUKO MOROGORO ! Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin