Monday, 4 May 2015

DULLY: HAJAOA, ANA WATOTO WANNE, KILA MMOJA NA MAMA YAKE

Mwana muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes.
Na Saphyna Mlawa
Dar es Salaam
UNAPOLITAJA jina la Dully Sykes katika ulimwengu wa Muziki wa Bongo Fleva hakuna shabiki wa muziki huo ambaye atasema hamfahamu kijana huyu aliyekulia mitaa ya Kariakoo na Ilala jijini Dar.
Mtindo wake wa majivuno na kujisifia ni kati ya vitu vilivyomfanya achukiwe na wengi, hali ambayo mwenyewe aliiona kama sifa kubwa ambayo ilisababisha kujiita Mr Misifa.
Dully Sykes akiwa katika pozi.
Kwa sasa utafanya kosa kubwa kama utaacha kulijumuisha jina la Abdul Abass Sykes, lililoibuka miaka ya 2000, ambalo lilizaa ‘Dully Sykes’ kama mmoja wa wakongwe kunako tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva.
Vibao kama Salome, Leah, Hi, Mr Misifa, Nyambizi, Bijou, Julietha na Bongo Fleva ndivyo vilivyochangia kumfanya kutambulika na kutamba sokoni.
Mkongwe huyo sasa anatamba na Kibao cha Shuka, ambaye pia ni mmiliki wa Studio ya Dhahabu Records iliyopo Tabata Bima jijini Dar.
Championi Jumatatu linakupa zaidi baada ya kumkalisha mkali huyo kilingeni.

Watoto wa Dully Sykes.
Hivi karibuni ulitoa wimbo mpya, mashabiki wameupokeaje?
Dah! Kwanza naomba niwashukuru mashabiki wangu ambao wamekuwa chachu ya maendeleo kwenye kazi zangu za muziki, huwezi amini ‘single’ niliitoa hewani Jumatatu iliyopita na kusambaza video siku ya Ijumaa lakini matumaini ni makubwa, kwa sababu wengi wameshaisikiliza na ninatumaini kupata ‘feedback’ nzuri.
Hata hivyo kuna kazi yangu ambayo nitaiachia hewani ‘soon’ nimefanya na Diamond na msanii flani hivi wa mbele ‘amazing’ ila siwezi kumtaja kwani ni mapema mno halafu nataka iwe ‘surprise’ kwa mashabiki wangu.

Ile project ya wimbo wa kumuinua Chid Benz, iliishia wapi?
Tayari wimbo upo ambao uliimbwa na Diamond na AY, mimi nilihusika katika kuutengeneza kama ‘produza’ tu na mashabiki wameupokea vizuri sana.
Chid Benz ni ndugu yetu, ndiyo maana tulianzisha ile project kwa ajili ya kuhakikisha anaachana kabisa na matumizi ya madawa ya kulevya, huu ni mwanzo tu, bado kuna mengine tutayafanya kwa ajili yake.

Studio yako inasaidiaje kuwainua wasanii wachanga?
Aisee kwa sasa nimesimama kufanya hizo shughuli za kuinua vipaji vya wasanii chipukizi kwa sababu kama ni kuwasaidia nimeshawasaidia sana lakini wengi wameniangusha.
Muda huu naangalia zaidi mambo yangu ya msingi, umri unaposonga na majukumu yanaongezeka! So acha nifanye yangu kwanza lakini sitaacha kuwasaidia kwa kuwa na mimi nilitokea huko, najua changamoto wanazokutana nazo.

Kifo cha baba yako kiliathiri vipi kazi zako?
Kiukweli kuondoka kwa mzee kwangu ni pigo kubwa sana, alikuwa ni zaidi ya rafiki yangu na mara kwa mara alikuwa akinishauri, kunionya na kunionyesha njia sahihi pale ninapokwenda tofauti. Lakini hilo naomba tusiliongelee sana maana kazi ya Mola haina makosa.

Vipi umewahi ‘kutoka’ na staa mwe-nzako?
Ha! Ha! Haaa! No, sijawahi ‘kudeti’ na staa na wala sitarajii, maana hao mastaa wenyewe sijaona hata wa kudeti naye.
Hata hivyo mimi bado sijaoa, lakini nitakapompata ‘wife material’ nitaoa tu, hata hivyo nina watoto wanne na kila mtoto ana mama yake. Mwanangu wa kwanza anaitwa Titho Sykes, naishi naye nyumbani kwangu.

Kitu gani unakichukia kwenye muziki?
Kikubwa zaidi ambacho ninachukia ni wivu na chuki zisizo na msingi baina ya wasanii. Hapa napenda kuwashauri wasanii wenzangu tupendane, pia ushirikiano ni muhimu kama tunahitaji kazi zetu zifike mbali zaidi.
Tujifunze kupitia kwa wenzetu lakini tukiendekeza mambo hayo, mafanikio yataendelea kuwa ya mtu mmoja-mmoja na siyo muziki kwa ujumla.

Unamzungu-mziaje Diamond hapa alipofikia?
Nichukue nafasi hii kumpongeza kwa mafanikio makubwa aliyoyafikia, kupitia yeye natumaini muziki wetu umejulikana zaidi kimataifa na nchi nyingi zimetujua kuwa nasi tunaweza.
Naamini amesaidia kufungua njia kwa wengine na utaona hata sasa kila msanii anataka kazi yake iwe kwenye ubora, jambo linalofanya tuzidi kupiga hatua.
Pia napenda kuipongeza kampuni yenu (Global Publishers Ltd) na ‘media’ mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanya kazi kubwa kusapoti kazi zetu za nyumbani! Siwezi kuwasahau pia mashabiki wangu ambao kwa namna moja au nyingine wamenifikisha hapa nilipo, lakini hata washikaji zangu wote ninawapenda, maana sina bifu na msanii hata mmoja.

DULLY: HAJAOA, ANA WATOTO WANNE, KILA MMOJA NA MAMA YAKE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin