Monday, 11 May 2015

ATAPELI KWA KUTUMIA DOLA ZA MAREKANI, ACHEZEA KICHAPO


Stori: Saimeni Mgalula, Mbeya
MAKUBWA! Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, mkazi wa Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya, amechezea kipigo cha ‘kufa mtu’ kufuatia madai ya kutaka kumwibia kwa kutumia dola za Kimarekani mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Anna.
Akiwa mikononi mwa polisi.
Tukio hilo la aina yake, lilijiri muda wa asubuhi, hivi karibuni maeneo ya Kisimani katika mji wa Tunduma.
Wakizungumzia tukio hilo, mashuhuda waliomchapa kijana huyo walisema inaaminika kwamba amekuwa na tabia hiyo ya wizi ambapo hudondosha kibunda cha ‘pesa’ chenye shilingi za Tanzania na dola za Marekani ili mpita njia akipita aokote kisha yeye kujitokeza kama wameokota wote hivyo kumwambia mpita njia huyo waende kichakani wakagawane, huko humpora kila alicho nacho.
“Siku ya tukio, huyu kijana alidondosha ‘fedha’ hizo ili amwingize mkenge mwanamke huyo lakini sisi wananchi kwa vile tunajua na tulimuona, tulimuwahi na kumuweka mikononi mwetu kisha kuanza kumpa kichapo.
“Huyu kijana hayupo peke yake, ana wenzake. Wakipita watu hudondosha hizo pesa, pindi utakapookota wewe pesa hizo wanakuchukua mpaka kwenye msitu wa idara ya maji kwa lengo la kugawana.
“Bila wewe kujua, unaingia tamaa na kwenda kugawana nao. Utakapofika huko wanakunyang`anya kila kitu na mbaya zaidi wanakupa kichapo,” alisema shuhuda mmoja.Kuhusu kijana huyo, mashuhuda walisema siku hiyo wangemfanyia kitu kibaya zaidi kama polisi wasingewahi kutokea na kumuokoa.

ATAPELI KWA KUTUMIA DOLA ZA MAREKANI, ACHEZEA KICHAPO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin