Monday, 18 May 2015

AIBU WASANII WANASWA KWA UFUSKA

SHABAASH! ‘Makinda’ wawili wanao penyapenya katika sanaa ya maigizo runingani wa Kundi la Sanaa la Jakaya Theatre Arts Group, Sefu Ngao ‘Stefano’ na Vanessa Msofe wamenaswa wakifanya uchafu kwa kuoneshana mahaba mazito huku wakiwa ‘bwii’, Ijumaa Wikienda linakupa ishu nzima.

Wasanii hao wakiwa katika mahaba mazito baada kulewa.
Tukio la uchafu huo unaotia kichefuchefu cha ‘mimba changa’, lilinaswa na ‘kiona mbali’ cha gazeti hili namba moja kwa skendo na ufuska wa wasanii, waigizaji na mastaa mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Sinza-Legho jijini Dar na kuzua mshangao mkubwa.
Wasanii hao wakiendelea na starehe zao....
Kitendo cha wasanii hao kufanya uchafu huo kisa ulevi, kilikatishwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo.
“Jamani nilipeni hela yangu na muondoke hapa,” alisikika mhudumu huyo aliyekerwa na vitendo vichafu vya wasanii hao.

AIBU WASANII WANASWA KWA UFUSKA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin