Tuesday, 14 April 2015

WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOTEKWA NIGERIA WAKUMBUKWA BAADA YA MWAKA 1


Wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na Boko Haram mwaka jana.
MAADHIMISHO ya mwaka mmoja tangu wasichana zaidi ya 200 kutekwa na Kundi la Boko Haram huko Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria yanafanyika leo Nigeria.
Wananchi wakiandamana kutaka kurudishwa kwa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na Boko Haram mwaka jana.
Wasichana zaidi ya 200 walitekwa Aprili 14, mwaka jana na kuitikisa dunia huku baadhi ya mataifa kama Marekani na China yakiahidi kusaidia upatikanaji wa wadada hao japo mpaka sasa bado hawajapatikana.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika Mji Mkuu wa Nigeria, Abuja huku wasichana 219 wakiwepo kuwakilisha wale waliopotea.
Michelle Obama akiwa na bango la #BringBackOurGirls.
Maadhimisho hayo pia yatafanyika sehemu nyingine kama London na Washington.
Jana Jumanne, Shirika la Amnesty International lilieleza kuwa wasichana na wanawake 2,000 wametekwa na Kundi la Boko Haram tangu kuanza kwa mwaka jana huku wakifanywa wapishi, watumwa wa ngono na wapiganaji.
Upoteaji wa wasichana hao ulipelekea kampeni ya #BringBackOurGirls iliyoenea katika mtandao wa Twitter huku ikiungwa mkono na watu mashuhuri duniani akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai.

WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOTEKWA NIGERIA WAKUMBUKWA BAADA YA MWAKA 1 Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin