Sunday, 26 April 2015

UMESIKIA HII YA MTOTO WA MIAKA 13 KUKUTWA MTUPU USIKU AKIWANGA, UNAAMBIWA ANAFUNGUA HADI KUFULI ZA MADUKA KICHAWI

Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amekamatwa usiku akiwa uchi kwa madai kuwa alikuwa akiwanga katika duka moja lililopo kijiji cha mpunguti Mkoa wa Mbeya.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mtoto huyo ni mzoefu kwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakipotelewa na fedha katika mazingira ya utata ambapo walitega mtego ili kubaini upotevu huo na kumbaini akiingia kwenye duka moja ambalo linadaiwa kuzindikwa.

Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa eneo hilo walidai taarifa za mtoto huyo ambaye alikuwa anaishi na bibi yake aliyemfukuza kutokana na tuhuma za ushirikiana na kukimbilia msituni kutokana na kukosa pa kuishi.

Inasemekana mtoto huyo aliishi misituni kwa zaidi ya miezi mitano ndipo aliporejea na kuolewa lakini ndoa yake haikudumu kutokana na maisha kuwa magumu na akaamua kuanza mbinu za kichawi kwa kuibia watu.


Alianza kufungua kufuli za maduka kwa kutumia kidole gumba huku akiwa uchi na alinaswa na kupelekwa kwenye ofisi za kata ambapo anashikiliwa hadi sasa.


UMESIKIA HII YA MTOTO WA MIAKA 13 KUKUTWA MTUPU USIKU AKIWANGA, UNAAMBIWA ANAFUNGUA HADI KUFULI ZA MADUKA KICHAWI Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin