Wednesday, 15 April 2015

PENNY, WEMA ETI WANA PROJECT


Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Wema  Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona habari za mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zali zinapamba moto kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la project.
Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’.
Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga kazi badala ya kupoteza muda.
Staa wa filamu Bongo, Wema  Sepetu.
“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki tena kushabikia mambo ya Zali na Diamond kwa sababu hayatuhusu,” alisema.

PENNY, WEMA ETI WANA PROJECT Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin