Tuesday, 14 April 2015

NDEGE ILIYOTAKIWA KUPELEKA ASKARI GARISSA ILIKUWA INATUMIWA KIFAMILIA


Ndanu Munene Mbithi (aliyevaa njano) ambaye ni mtoto wa Kammanda Rogers Mbithi, akiwa na rafiki zake kwenye ndege ya Jeshi la Polisi la Kenya.
NDEGE ya jeshi la anga la polisi nchini Kenya ambayo ilikuwa itumike kupeleka askari kwenye Chuo Kikuu cha Garissa wakati mauaji ya kigaidi yanaendeshwa dhidi ya wanafunzi, ilikuwa iko Mombasa ikitumiwa kwa mambo binafsi na kamanda wa jeshi hilo, Rogers Mbithi.
Sehemu ya ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa isafirishe askari wajulikanao kama ‘GSU Recce’ kwenda Garissa  siku ya Aprili 7, ambapo ilikuja kuonekana kwenye mtandao wa Instragram picha ya mmoja wa mabinti wa Mbiti wakiwa kwenye ngazi za ndege hiyo na maneno yaliyoandikwa:  "Mombasa ni raha tu".  Maneno mengine yaliyokwenda sambamba na picha hiyo yalikuwa ni: "Hi Mombasa...#birthdayweekend".
Mkuu wa jeshi la polisi (IGP), Joseph Boinnet, alikuwa amesema awali kwamba ndege hiyo haikuwepo ili kupeleka askari huko Garissa na amesema uchunguzi umeanzishwa ili kufahamu ndege hiyo ilikuwa wapi wakati magaidi wakiua wanafunzi 147

NDEGE ILIYOTAKIWA KUPELEKA ASKARI GARISSA ILIKUWA INATUMIWA KIFAMILIA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin