Saturday, 4 April 2015

KISA DIAMOND BODABODA ALA KICHAPO KITAKATIFU


DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Shabani ambaye ni dereva wa bodaboda wa Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Matombo Wilaya ya Morogoro Vijijini, amenusurika kifo baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi akidaiwa kugonga basi la wasanii waliotoka Dar kuja kushiriki mazishi ya marehemu Abdul Bonge kijijini hapa.
Bodaboda huyo akiamuliziwa baada ya kupewa kichapo
Kwa mujibu wa chanzo, bodaboda huyo aligonga basi hilo dogo aina ya Toyota Coaster sehemu ya mbele alipokuwa akijaribu kuyakwepa magari mengi yaliyofurika eneo hilo la msiba ambapo inadaiwa alipoteza umakini baada ya kumuona Diamond ndipo akagonga.
bodaboda iliyosababisha ajali.
Baada ya kutokea ajali hiyo, umati wa watu ulitoka msibani na kwenda kumshushia kichapo bodaboda huyo kama fundisho kwani ilidaiwa kuwa madereva wengi wa bodaboda kijijini hapa wana kasumba ya kuendesha kwa kasi bila uangalifu.
Sehemu ya mbele ya basi dogo aina ya Toyota Coaster baada ya kugongwa na bodaboda.
“Hawa wanaleta masihara sana barabarani, wanaendesha kwa fujo, hawapo makini sasa dawa yao ni kuwakong’ota wapate adabu,” alisikika jamaa mmoja aliyekuwa akimpa kipondo bodaboda huyo.i
Hata hivyo,  shuhuda mmoja alimtetea bodaboda huyo kwa kusema hakugonga kwa makusudi lakini aliyemponza ni Diamond.
Diamond akicheka baada ya kupewa taarifa hiyo.
“Alikuwa anamshangaa Diamond huku anaendesha ndipo akagonga,” alisema shuhuda huyo.
Baada ya kumpa kipigo hicho, mwanahabari wetu alimshuhudia dereva wa basi hilo akishirikiana na wenzake wakimchukua bodaboda huyo na pikipiki yake hadi Kituo cha Polisi Mkuyuni ambako walifanya mazungumzo ili bodaboda huyo alipe fedha za matengenezo ya gari hilo.

KISA DIAMOND BODABODA ALA KICHAPO KITAKATIFU Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin