Monday, 6 April 2015

BOZI: NAY WA MITEGO ANA LAANA YANGUMSANII wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.

Muuza nyago kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.
Emmanuel Elibariki ‘Nay’
“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye mitandao ya kijamii,  jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.

BOZI: NAY WA MITEGO ANA LAANA YANGU Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin