Saturday, 18 April 2015

BETHIDEI YA MTOTO WA DAVINA NISHA ATIA AIBUPOMBE si chai! Msemo huu ulitimia hivi karibuni baada ya staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kuzidiwa na kilevi na kuanza kushindana kukata mauno na kusababisha azingirwe na wanaume waliovutiwa naye.

Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ akikata mauno.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano iliyopita katika sherehe ya bethidei ya mtoto wa msanii mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ iliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Lamada jijini Dar ambapo kulikuwa na vyakula na vinywaji vikali vya kila aina.
Nisha ambaye alikuwa amevalia kikaptula cha ‘jeans’ na kujistiri na mtandio, baada ya kukolea ulevi aliutupa mtandio na kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi kisha  kukata mauno kushindana na mademu mcharuko waliokuwa ukumbini hapo kiasi cha kuwapagawisha wanaume wakware ambao walimvaa na kutaka kucheza naye.

Davina akiwa na mwanaye.
“Duh yaani Nisha leo ametia aibu, si kawaida yake nahisi mitungi imemzidi. Ameamua kujiachia kupitiliza, hebu mwangalie anavyokata mauno watoto wanamuangalia, aibu hii,” alisikika mualikwa mmoja akimwambia mwenzake.
Mauno mauno.
Hata hivyo, Davina alipoona baadhi ya waalikwa wanazidisha kusaula na kukatika, aliomba kipaza sauti na kuwataka wasifanye hivyo kwani sherehe ni ya mtoto.Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Mayasa  Mrisho ‘Maya’, Mike Sangu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi ambao  baadhi yao walionekana wakiwa wamekolea kilevi

BETHIDEI YA MTOTO WA DAVINA NISHA ATIA AIBU Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin