Sunday, 19 April 2015

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI AKIVUKA RELI HUKO MOROGORO


Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kugongwa vibaya na treni wakati akivuka reli na kisha viungo vyake kusambaa katika mtaa wa ujenzi Manispaa ya Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alijulikana kwa jina moja la Mangi ambapo wameeleza kusikitishwa na ajali kwa kuwa hii ni mara ya tatu watu kugongwa na treni katika maeneo hayo na kueleza kuwa amarehemu alikuwa anavuka reli.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa ujenzi Christopher Charles ameelezea tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kupita kwenye njia ya Reli kwani wataendelea kusababisha ajali zisizo za lazima ambazo zingeweza kuepukika. 

Askari wa jeshi la polisi wamefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu ambapo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Via>>ITV

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI AKIVUKA RELI HUKO MOROGORO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin