Friday, 6 March 2015

UKATILI TENA: HAUSIGELI MWINGINE AJERUHIWA VIBAYA NA BOSI WAKE


Majeraha aliyonayo kichwani Melina Mathayo baada ya kupigwa na bosi wake.

HAUSIGELI aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15, ameumizwa vibaya sehemu za kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na bosi wake aitwaye Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.
Akiongea na mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina amesema amekuwa akipigwa na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia waya, brenda na vifaa vingine japo alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo hivi vya ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku chache baada ya hausigeli aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi wake aitwaye Amina Maige aliyepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti huyo aliyeletwa Mwananyamala leo alfajiri akiwa na hali mbaya amefanya kazi kwa miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani Kagera.
Melina alikuwa akiongea na mwanahanbari wetu akiwa na mpira wa kuongezewa damu mwilini na amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea tukio hilo.

UKATILI TENA: HAUSIGELI MWINGINE AJERUHIWA VIBAYA NA BOSI WAKE Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin